Kanye West ana wasiwasi mwanae ataangukiwa na ‘drones’ zitakazotumiwa na mapaparazzi kupata picha zake!



Kwa mujibu wa Kanye West, Mapaparazzi ni hatari zaidi kuliko hata Nazi! Uoga wake huo wa mapaparazzi umemfanya staa huyo atafute nyumba yenye thamani ya dola milioni 20 ili kuwakwepa wasipate picha za mwanae North.



North West

Hivi karibuni Kanye alikuwa akihojiwa (deposition) na mawakili wa paparazzi aliyemdunda na kujikuta akitoa kauli iliyowaacha mdomo wazi. Kanye anahisi kuwa mapaps wataisaka picha ya binti yake North anayemlea kama yai kwa udi na uvumba hata ikibidi kutumia ndege zinazoondeshwa kwa remote control maarufu kama drones ili zipate picha yake.

0 comments:

Post a Comment