
Monagangstar
Producer Monagangstar aliyeripotiwa kuwa ndiye msimamizi wa kazi za Young Killer amesema kuna mambo tofauti anafanya rapper Young Killer yanayoashiria utovu wa nidhamu na kinyume na mkataba. Monagangstar anasema Kuna kitu kipo tofauti na tulivyoanza kufanya kazi Na Young Killer…..
“Young Killer amebadilika,amekuwa maarufu na ameshikwa masikio na watu, Bado nina mkataba na Young Killer mpaka December 2014 ila anaukiuka mkataba huu kwa kwenda kufanya kazi studio zingine na sasa hata Classic Sounds hafiki, Classic Sounds haim’bani msanii ila akitaka kufanya kazi nje ya studio hii ni lazima tubaki kama Executive Producer wa kazi hio ilituhakikishe kiwango cha kazi ni bora, Young Killer amefanya kazi nje ya studio bila taarifa wakati mkataba wa Classic Sounds hauruhusu hicho kitu” Alisema Monaganster

Young Killer Na Monagangstar Kwenye Tuzo Za Kili 2014
Hii sio mara ya kwanza kusikia taarifa za kutofautiana kwa Young Killer na Monagangstar, kama wiki chache nyuma palikuwa na uvumi kuwa wawili hawa hawafanyi kazi pamoja na Young Killer alivunja mkataba. Young Killer amefanya kazi yake mpya studio za Combination Sounds kwa Man Water, Kazi mpya inaitwa Umebadilika na ameshirikishwa Banana Zoro.
0 comments:
Post a Comment