Rihanna anahisi Drake na Chris Brown bado wana harufu ya maziwa ya mama zao, na Eminem ndiye mwanaume halisi.
Rihanna, 26, yupo kwenye ziara ya pamoja na Eminem, 41, Monster na kwa mujibu waHollywoodLife.com, Riri anapenda kupanda jukwaani na Eminem na anadai kuwa ni muda mrefu tangu atumbuize na ‘mshindi wa kweli’.
Kwa mujibu wa vyanzo vilivyoongea na mtandao huo, ziara na Eminem inampa Rihanna maisha kwakuwa rapper huyo ni mtu mzima na muelewa. Chanzo hicho kimesema kuwa Rihanna Drake na Chris wana wivu kwasababu hawawezi kuwa naye.
Hivi karibuni Drake alidaiwa kumdiss Rihanna kwa kumfananisha na shetani.
0 comments:
Post a Comment